Julius Nyaisanga afariki Dunia
20 Oktoba, 2013 \\ Maoni Nyaisanga

Ni kwa masikitiko makubwa sana tunatangaza kifo cha mtangazaji wa siku nyingi Julius Nyaisanga (Pichani: wa Kwanza Kulia).

Taarifa zilizopokelewa asubuhi ya leo kutoka Morogoro zinathibitisha kufariki kwa aliyekuwa mtangazaji wa Radio One na Radio Tanzania inayofahamika sasa kama TBC Taifa Julius Nyaisanga ambaye hadi umauti unamfika alikuwa akifanya kazi na Abood Media ya mjini Morogoro kama meneja wa kituo cha Redio Abood FM.

Taarifa hizo zimethibitisha pia kuwa Nyaisanga aliyefahamika zaidi kama ‘Uncle J’ amefariki kutokana na presha pamoja na kisukari, magonjwa ambayo yamekuwa yakimsumbua kwa muda mrefu.

Tutaendelea kukujuza zaidi kadri tutakavyopata taarifa zaidi.

RIP Uncle J…